Mbali na kufunga bao zuri, Chama anaendelea kuonyesha dalili za kurejea kwenye ubora wake wa zamani.
Katika dabi ya Kombe la Muungano, alisababisha penati ya ushindi. Katika mchezo huu wa ligi, amefunga bao moja na kutoa pasi ya bao kwa Libasse Gueye.
Hii inaonyesha wazi mchango wake katika mechi kubwa na uwezo wake wa kuamua matokeo.

“Chama atabaki kuwa mtu wa ajabu kuwahi kucheza soka la Tanzania”
“Kwenye jumba la makumbusho na historia ya soka Tanzania, jezi ya Clatous Chama itapambwa na madini ya dhahabu na almasi. Mwamba kutoka Lusaka amedhihirisha kuwa yeye ni mchezaji wa daraja la juu sana”.
Kwa kiwango hiki, Chama anaendelea kuthibitisha hadhi yake kama mchezaji wa mechi kubwa. Anazeeka na ubora wake.






Leave a Reply